BENJAMIN NETANYAHU AKANUSHA MADAI YA UJASUSI DHIDI YA MAREKANI
Netanyahu akanusha taarifa inayodai Israel
kuhusika na ujasusi dhidi ya Marekani
Ripoti hiyo imeeleza kuwa maafisa
watatu wazamani wa Marekani ambao wanasema kuwa Israel ilikuwa inahusika kuweka
kifaa karibu na ikulu ya Marekani.
Lakini maelezo kutoka katika
ofisi ya Netanyahu imekanusha kutohusika kwa namna yoyote.
"Israel ina majukumu mengi
ya kuyafanyia kazi nchini mwake hivyo haiwezi kujihusisha na shughuli za
ujasusi nchini Marekan
Rais Donald Trump, aliulizwa na
waandishi wa habari siku ya alhamisi kuhusu ripoti hiyo ya ujasusi naye alisema
kuwa aamini kama Israel ilikuwa inaipeleleza Marekani .
"Inaniwia vigumu kuamini
kuwa Israel wana tuchunguza kwa sababu tuna uhusiano mzuri," Rais Trump
alisema.
alisema pia kuwa mwishoni mwa
majadiliano ya mkataba wa nyuklia na viongozi wa Marekani wamekuwa wakipingana
katika kuhamisha ubalozi wa Marekani katika mji wa Jerusalem.
"Siwezi kuamini hiyo stori,
kila kitu kinawezekana lakini siamini."
Wasajili wa kimataifa wa simu za
mkononi, ambao wanafahamika kama 'StingRays' waliripoti kuwa walipatikana
katika maeneo karibu na makazi ya rais na maeneo mengine nyeti katika mji wa
Washington DC wakati wa utawala wa Trump.
Vifaa hivyo vinafanana na simu za
mkononi vilitumwa katika maeneo yao na kuweza kupata taarifa zote za simu
zinazotumika katika eneo hilo.
Afsa mmoja wa zamani alizungumza
bila kutaja jina lake na kusema kuwa 'StingRays' ilitengenezwa kwa mfumo wa
kufanya ujasusi dhidi ya rais Trump.
Hakusema kama walifanikiwa.
Shirika la kijasusi la FBI,
linafanya uchunguzi ili kubaini vifaa hivyo vimetoka wapi.
" Jambo liko wazi kabisa
kuwa Israel ilikuwa inahusika,"
Afisa huyo wa zamani masuala ya
ujasusi alieleza.
Na kiongozi huyohuyo alikosoa
uongozi wa Trump kuwa awajawajibika na ujasusi huo.
Comments
Post a Comment