IRAN KUSHUTUMIWA NA MAREKANI KUSHAMBULIA HIFADHI YA MAFUTA SAUDIA
Marekani yasema Iran ilikuwa
nyuma ya mashambulio ya hifadhi ya mafuta ya Saudia
Iran inakana kuhusika na mashambulio hayo ya ndege , ambayo
yalidaiwa kutekelezwa na waasi wa kiuhudhi wanaounga mkono Iran nchini Yemen.
lakini maafisa wa Marekani ambao hawakutajwa majina wakizungumza
na vyombo vya habari vya kimataifa nchini Marekani wamesema eneo na ukubwa wa
mashambulio vinaonyesha kuwa Wahudhi hawakuhusika na mashambuli hayo.
Tukio hilo lilisababisha kupungua kwa mauzo ya mafuta
duniani kwa 5% na limesababisha kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo.
Marekani inasema nini ?
Waziri wa ulinzi wa Marekani Mike Pompeo aliilaumu Iran wikendi
bila kutoa ushahidi wowote , jambo lililoichochea serikali ya Tehran kuushutumu
utawala wa Washington kwa uongo.
Katika ujumbe wake alioutoa kwneye mtandao wa kijamii wa Twitter
siku ya Jumapili, rais Donald Trump hakuishutumu moja kw amoja Iran, lakini
alisema kuwa hatua za kijeshi zinaweza kuchukuliwa pale muhusika wa mashambulio
atakapojulikana.
Maafisa wa Marekani wamekuwa wakizungumza na na
mvyombpo vya habari kama vile New York Times, ABC na Reuters.
Afisa mmoja amesema kuwa kulikuwa na vituo 19 vilivyolengwa na
mashambalio , na kwamba mashambulio hayo yalitokea upande wa magharibi-
kaskazini - na magharibi tena - si upande wa eneo linalodhibitiwa na waasi wa
kihudhi nchini Yemen, ambalo liko Kusini -magharibi mwa vituo hivyo
vilivyoshambuliwa
Maafisa wanasema kuwa kutokana na mwelekeo wa maeneo yalikotokea
mashambulio inaonyesha kuwa washambuliaji walikuwa katika Ghuba , Iran au Iraq.
Picha zilizoonyesha uharibifu mkubwa uliofanywa matanki ya kutengeneza mafuta
upande wa magharibi mwa vituo hivyo katika eneo la Abqaid
Iraq imekanusha kuwa ilihusika na mashambulio hayo ya wikendi
yalitokea kwenye ardhi yake . Waziri Mkuu wa IraqAdel Abdul Mahdi amesema kuwa
waziri wa ulizi wa Marekani Bwana Pompeo kwa njia ya simu alimhakikishia kuwa
Marekani inaunga mkono msimamo wa Iraq kuhusiana na tukio hilo.
Maafisa walionukuliwa na gazeti la New York Times
walinukuliwa wakisema mchanganyiko wa ndege zisizokuwa na rubani huenda
zilitumwa katika shambulio hilo, lakini sio zote zilizopiga maeneo
zilizoyalenga katika vituo vya mafuta vya Abqaiq na Khurais.
kituo ccha habari cha ABC kilimnukuu afisa wa ngazi ya juu wa
Marekani akisema kuwa Bwana Trump anaelewa fika kwamba Iran iliwajibika na
mashambulio.
Uchina na Muungano wa Ulaya wametaka pande
zinazozozana kuhusu mashambulio haya kuwa na subra.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Dominic Raab amesema kuwa
haijabainika wazi ni nani aliyehusika katika kile alichokitaja kama
"ukiukani mkubwa wa sheria za kimataifa ".
Masoko ya mafuta duniani
yameathirika kwa kiwango gani ?
Bei ya mafuta imepanda kwa kiwango ambacho hakijawahi kushudiwa
kwa siku moja tangu vita vya Ghuba vya mwaka 1991 , vikipanda kwa 20% lakini
baei hiyo ilishuka baadae.
Bei ya mafuta ghafi ilipanda hadi kufiki dola $71.95 kwa pipa
wakati mmoja.
Iran imejibu nini?
Iran haijasema lolote bado juu ya
kauli za sasa za Marekani .
lakini waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Javad
Zarf alituma ujumbe wa twitter Jumapili kumtuhumu Bwana Pompeo akisema kuwa
"Kwa kushindwa kukabiliana na shinikizo kubwa , waziri Pompeo amegeuka
kuwa muongo".
Alikuwa akizungumzia shinikizo lililotajwa na utawala wa Trump
kuhusu "kampeni yake ya shinikizo kubwa " ambalo liliilenga Iran kwa
vikwazo tangu Marekani ilipojiondoa katika mkataba wa kimataifa wa kidhibiti
mpango wa Iran wa nuklia .
Mashambulio ya Iran yalikuwaje ?
Mashambulio yalilenga kituo cha kutengeneza mafuta cha Abqaiq,
ambacho ni kiwanda kikubwa zaidi cha kutengeneza mafuta cha taifa la Saudia ,
Aramco, pamoja na machimbo ya mafuta ya Khurais
Khurais ni kituo kilicho karibu zaidi nampaka wa Yemen kikiwa
maili 480 kutoka mpakani.
Shambulio la ndege zisizokuwa na rubani lilichoma
hifadhi mbili za mafuta zinazomilikiwa na kampuni ya serikali ya taifa la
Saudia Aramco , kulingana na vyombo vya habari.
Kanda za video zilionyesha moto mkubwa katika eneo la Abqaiq
ikiwa ndio hifadhi kubwa ya mafuta ya Saudia huku shambulio la pili likichoma
moto hifadhi ya mafuta ya Khurais.
Msemaji wa kundi la Houthi linaloungwa mkono na Iran nchini
Yemen alisema kwamba walirusha ndege kumi zisizo na rubani katika shambulio
hilo.
Msemaji waasi hao Yahya Sare aliambia televisheni ya al-Masirah
ambayo inamilikiwa na waasi hao wa Houthi kwamba mashambulio zaidi yanafaa
kutarajiwa katika siku za usoni.
Alisema kwamba shambulio hilo la siku ya Jumamosi ndio kubwa
zaidi kuwahi kutekelezwa na wapiganaji hao ndani ya Saudia na kwamba
lilitekelezwa kupitia usaidizi wa baadhi ya raia wa ufalme huo.
Maafisa wa Saudia hawajatoa tamko lao kuhusu ni nani
wanayefikiria alihusika na shambulio hilo.
Comments
Post a Comment