KAULI ZA MWANAUME KUKUCHOKA
Leo mpenzi msomaji wa safu hii, nimekuja na mada mpya ambayo imenisukuma kuwaandikia wanandoa na wapenzi walioko kwenye uhusiano kwa muda mrefu kwani wengi hujikuta wameachwa na kuona kuwa ni ghafla kumbe hawakutambua kwa kujua ni utani. Kauli anazozitoa mwanaume wako ni wazi kabisa kuwa amekuchoka wengi hawazitambui sasa zisome kwa makini na uzielewe. Tukiachana sisi si wa kwanza Kauli kama hii mwanaume hawezi kukuambia mkiwa kwenye mapenzi kwa mara ya kwanza, hivyo ni lazima kwa kukutamkia hivyo ujue moja kwa moja umechokwa. Hivi ni nani ambaye hajui kuwa mapenzi ni malumbano ya mara kwa mara hata kwa vitu vidogo? Kama hampendani hamuwezi kutofautiana kwani mtakutana wapi au mtakutanishwa na nani hasa? Ulipoingia kwenye penzi kwa mara ya kwanza hata alipokuwa akikukwaza uliomba yaishe mapema na wala hukuwahi kufikiria kukwambia kuwa tukiachana sisi si wa kwanza, ulitumia nafasi yako kikamilifu kwa kumbembeleza na akakuelewa mkamaliza mzozo. Ipo siku utajutia ...