KAULI ZA MWANAUME KUKUCHOKA
Leo
mpenzi msomaji wa safu hii, nimekuja na mada mpya ambayo imenisukuma
kuwaandikia wanandoa na wapenzi walioko kwenye uhusiano kwa muda mrefu kwani
wengi hujikuta wameachwa na kuona kuwa ni ghafla kumbe hawakutambua kwa kujua
ni utani.
Kauli anazozitoa mwanaume
wako ni wazi kabisa kuwa amekuchoka wengi hawazitambui sasa zisome kwa makini
na uzielewe.
Tukiachana
sisi si wa kwanza
Kauli kama hii mwanaume
hawezi kukuambia mkiwa kwenye mapenzi kwa mara ya kwanza, hivyo ni lazima kwa
kukutamkia hivyo ujue moja kwa moja umechokwa.
Hivi ni nani ambaye hajui
kuwa mapenzi ni malumbano ya mara kwa mara hata kwa vitu vidogo? Kama
hampendani hamuwezi kutofautiana kwani mtakutana wapi au mtakutanishwa na nani
hasa?
Ulipoingia kwenye penzi kwa
mara ya kwanza hata alipokuwa akikukwaza uliomba yaishe mapema na wala hukuwahi
kufikiria kukwambia kuwa tukiachana sisi si wa kwanza, ulitumia nafasi yako
kikamilifu kwa kumbembeleza na akakuelewa mkamaliza mzozo.
Ipo
siku utajutia hili penzi
Maana yake nini? Mpaka
mnafikia hatua anakwambia hivyo ni wazi anashindwa kujitoa lakini pia anao
uwezo wa kujitoa hivyo anakuandaa kisaikolojia.
Kwa mtu unayempenda kwa dhati
huwezi kumwambia ipo siku atajutia penzi ni neno lisilostahili kwa mpenzi wako,
ukiona unaambiwa hivyo jua siku zako zinahesabika.
Afu
we mwanamke una mdomo sana
Ukiona mpenzi wako anakerwa
na mdomo wako mara kwa mara na anakutamkia jua wazi mapenzi hakuna. Wanaume
wengi hawapendi mwanamke anayeongea hasa kama anamkosoa kwa jambo fulani.
Mfano kama kuna vitu ulikuwa
ukimwambia mwanzo anakubali na kuendana na wewe lakini akishakuchoka ukiongea
tu anakuona kero, hii pia ni dalili ya kuachwa.
Kwani
nilikukuta mtoto, tumejuana ukubwani
Wanaume wengi wanapenda
kutumia kauli hii pale wanapowachoka wapenzi wao hasa wanapokuwa kwenye
malumbano, bila shaka msomaji utakuwa na ushahidi wa hili hasa kwa wale
waliowahi kukutana na maneno haya wataniunga mkono.
Ni maneno yanayouma na
kujirudia kwenye ubongo wa mwanamke pia hupunguza mapenzi kwani mwanamke
akitamkiwa hivyo mara kwa mara hujikuta ubongo unaanza kukubali na kupunguza
mapenzi kwa yule aliyekuwa akimpenda.
Kwa
wanaume wote
Kama bado unampenda
mpenzi/mkeo kamwe usimtamkie maneno haya ni sumu kubwa, huenda unatamka kwa
bahati mbaya unapokuwa na jazba lakini yamekuwa yakiwaumiza wenza wenu na
wakiamua kuachana nanyi watawachukia milele.
Comments
Post a Comment