HAMZA BIN LADEN: KUTHIBITISHWA AMEUWAWA
Hamza Bin Laden: Trump
athibitisha kuwa mwanawe kiongozi wa al- Qaeda ameuawa
Mwezi uliopita vyombo vya habari vya Marekani vilinukuu duru za
kijasusi ambazo ziliripoti kwamba aliuawa katika shambulio la angani.
Alitajwa na Marekani kuwa gaidi miaka miwili iliopita.
Alionekana kuwa mrithi wa moja wa moja wa babake.
Akidaiwa kuwa na umri wa miaka 30 alikuwa ametoa wito
wa mashambulizi dhidi ya Marekani na mataifa mengine.
''Hamza Bin Laden kiongozi mkuu wa al-Qaeda na mwana wa Osama
bin Laden aliuawa katika shambulio la operesheni ya Marekani dhidi ya ugaidi
nchini Afghanistan / Pakistan''.
Bwana Trump alizungumza katika taarifa fupi iliotolewa na Ikulu
ya Whitehouse.
Kifo cha Hamza kinainyima Al - Qaeda uongozi muhimu na uhusiano
wa babake lakini pia kinakandamiza operesheni na vitendo vya kihalifu vya kundi
hilo.
Taarifa hiyo haikutoa mda wa operesheni hiyo. Mwezi Februari
Marekani ilikuwa imetoa ofa ya $1m kwa habari ambayo ingepelekea kukamatwa kwa
Hamza
Hamza Bin Laden alionekana kuwa kiongozi chipuka wa al- Qaeda .
Iliripotiwa mwezi Agosti kwamba alikuwa ameuawa na operesheni ya
kijeshi katika kipindi cha miaka miwili iliopita na serikali ya Marekani
ilihusika lakini muda na tarehe haikujulikana..
Wasifu wa Osama bin Laden
Bin Laden aliwahi kunukuliwa akisema: "Kile ambacho
Marekani inakionja hivi leo ni kitu kidogo sana ikilinganishwa na kile ambacho
tumekuwa tukikipata katika miongo kadhaa. Taifa letu limekabiliwa na hali hii
ya kudhalilishwa na kudharaualiwa kwa zaidi ya miaka 80. Wanawe wanauwawa, damu
yao inamwagwa, maeneo yake matakatifu yanahujumiwa na hayatawaliwi kwa mujibu
wa amri zake Mwenyezi Mungu."
Osama bin Laden alizaliwa mwaka 1957 katika familia yenye
utajiri mkubwa. Baba yake alianzisha kampuni kubwa ya ujenzi katika Saudi
Arabia. Akiwa ni miongoni mwa ndugu 18 wa kiume, Osama aliwahi kufanya kazi
katika biashara hiyo ya familia. Maisha yake yalianza kubadilika alipokuwa
kijana pale Muungano wa Sovieti ulipoivamia Afghanistan.
Alipokwenda Aghanistan, Osama alikuwa kijana sana ambaye alitaka
kujijengea umaarufu, katikati ya vita vitakatifu. Osama bin Laden alikaa kwa
kipindi cha takriban miaka 10 nchini Afghanistan, na kuanzisha fungamano na
wanaharakati wa siasa kali za kiislamu kote duniani.
Na baada ya majeshi yaliyovunjika moyo ya Sovieti kuondoka
Afghanistan mnamo mwaka 1989. Osama bin Laden alirejea nyumbani Saudi Arabia.
Mwaka mmoja baadaye alijitolea kumpa msaada wa kijeshi mfalme Fahad wakati Iraq
ilipoivamia nchi jirani ya Kuwait. Lakini Osama alipatwa na mshtuko mkubwa pale
Mfalme Fahad alipokataa toleo lake na badala yake kuigeukia Marekani.
Osama alinyaganywa uraia wa Saudi na akarejea Afghanistan ambayo
wakati huo ikitawaliwa na Wataliban ambao alikubaliana nao kuhusu tafsiri ya
uislamu.
Mnamo mwaka 1998 aliwahimiza waislamu wawauwe Wamarekani mkiwemo
raia popote pale watakapowapata, kukafuatiwa mashambulio kadhaa ikiwa ni pamoja
na dhidi ya balozi za Marekani katika Kenya na Tanzania na manowari ya USS Cole
katika mwambao wa Yemen. Halafu shambulio la September 11, 2001.
Comments
Post a Comment