KIJUE KILIMO STRAWBERRY NA SOKO LAKE
strawberry (fukasidi) hustawi katika maeneo yenye joto la wastani, na
hukua kwa haraka zaidi na uzalishaji kuongezeka linapolimwa kisasa zaidi, Hasa
katika Green house. Zao hili hukua vizuri katika mwinuko wa mita
1500 na zaidi kutoka usawa wa bahari. Zao hili hata Tanzania hustawi zaidi
katika mikoa mingi kama Morogoro,mbeya,iringa, Arusha, Kilimanjaro, na Pia
hufanya vizuri katika mikoa ya Pwani endapo utalima kisasa zaidi na kufuata
maelekezo ya kitaalamu(Under controlled condition)
Udongo
strawberry inaweza kustawi vizuri kwenye udongo tifutifu wenye
rutuba. Zao hili haliwezi kustahimili ukuaji kwenye udongo wenye chachu
nyingi, hasa chokaa kwani mizizi yake huoza kwa urahisi, Pia udongo
unaotuamisha maji kama mfinyanzi sio mzuri sana kwa ustawishaji wa strawberry,
Pima Udongo kabla ya kuanza kilimo sio kwa strawberry peke yake hata kwa mazao
mengine
Kupanda
Ili kuwa na mazao bora ambayo yatakuwezesha kupata
soko la uhakika, inashauriwa kuzalisha kwenye nyumba maalumu ya
kuzalishia mazao (green house).
1. Katika upandaji wa strawberry kwenye green house
Utahitajika kuwa na Mabomba yenye matundu(Plastic Pipe)
Matundu katika bomba hilo yawe na
umbali wa inchi 1.
2. Ni vyema matundu hayo yakawa zigzag, ili kuruhusu mimea utakayoipanda kukua vizuri bila kusongamana
2. Ni vyema matundu hayo yakawa zigzag, ili kuruhusu mimea utakayoipanda kukua vizuri bila kusongamana
3.
Tandika karatasi la nylon sakafuni ili kuwezesha maji utakayotumia kunyeshea
kurudi kwenye bwawa au
sehemu ya kuhifadhia.
4.Ning’iniza mabomba hayo kwa kutumia waya.
5. Jaza kokote,
yenye mapande makubwa kiasi.
6 .Panda miche
kwenye kila tundu kwa uangalifu ili mizizi isikatwe na kokoto zinazoshikilia
mme Kupanda
Kwenye Shamba la Kawaida
umwagiliaji
Mimea ya strawberry inahitaji maji kwa kiasi kikubwa sana. Hii
inamaanisha kuwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri
wa umwagiliaji kabla ya kuanza kilimo cha zao hili. Unapaswa kumwagilia
mara nne kwa siku, kila baada ya saa nne unapaswa kumwagilia kwa robo saa. Hii
itawezesha mimea yote kupata maji ya kutosha. Endapo stroberi haitapata maji ya
kutosha, uzalishaji wake pia utakuwa ni hafifu sana, kwani maua hayatachanua
ipasavyo na hata matunda kukomaa inakuwa ni shida.
Kuvuna
Zao la strawberry huzaliana na kukomaa kwa haraka sana. Unaweza
kuanza kuvuna stroberi baada ya mwezi mmoja tangu kupandwa. Kila wiki stroberi
inakuwa na matunda mapya, na kila tunda likishatokeza huiva kwa haraka, hivyo
uvunaji wake ni wa mfululizo ikshafikia hatua hiyo tegemea kuwa na wiki 2-3 za
kuvuna mfululizo.
Kwa kuwa matunda ya stroberi ni laini, epuka kushika tunda wakati wa
uvunaji ili lisiharibike. Shika kikonyo
cha tunda ili kuvuna kwa usalama. Usiache matunda yaliyoiva shambani kwa
muda mrefu kwani yanaweza
kusababisha mimea kuoza. Pia yatapoteza ladha na virutubisho halisi
vinavyotakiwai
Wadudu na magonjwa
Endapo strawberry inazalishwa kwenye nyumba maalumu ya mimea, hakuna
magonjwa wala wadudu wanaoishambulia. Ikiwa mkulima anazalisha stroberi kwenye
eneo la wazi, stroberi inaweza kushambuliwa na magonjwa ya ukungu, pamoja na magonjwa
yanayosababishwa na virusi. Kama vile;
( Wadudu
b. Heliothis
f. Aphids
( Magonjwa
Lethal yellows
Mmea ulioathirika unaonyesha dalili zifuatazo;
Majani yaliyokomaa yanakuwa na
rangi ya dhambarau na yanajinyonganyonga kwa upande wa juu na kusababisha
kuangua chini.
Majani chipukizi yanakuwa na rangi ya njano katika
kingo za jani na kupelekea kudumaa kwa kikonyo cha jani. Huu ugonjwa unapunguza
nafasi ya jani kushindwa kujitengenezea chakula chake na hivyo mmea kudumaa na
kupelekea kufa kwa mmea.
Mnyauko
fusari (fusarium wilt)
Huu ugonjwa huunezwa na mbegu zenye huu ugonjwa na
husambazwa na vimelea vya fangasi ambavyo vipo kwenye udongo.
Ugonjwa huu hujitokeza Zaidi kwenye kipindi cha
kiangazi na hushambulia sehemu za mirija yam mea ya kupitishia chakula hivyo
mmea hukosa chakula na maji na hatimaye unyauka na kufa. Na shina la mmea
ukipasua ndani unakuta lina rangi ya kahawia.
Kudhibiti
1. Tumia mbegu safi na bora.
2. Tumia dawa ya kuua wadudu na magonjwa
ili kupata mazao mengi na yenye ubora.
3. Choma masalia ya mazao ili kudhibiti
uenezaji wa ugonjwa
4. Chagua mbegu ambayo ina uwezo wa
kuhimili magonjwa.
Matumizi ya strawberry
Matunda ya strawberry yana matumizi mbalimbali kulingana na uhitaji wa
mtumiaji, jamii na maeneo.
Miongoni mwa matumizi hayo ni pamoja na
-
Kuliwa kama tunda
- Kutia
ladha katika aina mbalimbali za vyakula.
- Kuweka
rangi, harufu na nakshi katika vipodozi.
- Kutengeneza
marashi n.k.
strawberry inapooteshwa kwenye greenhouse hutoa mavuno mengi na
yenye ubora. Wasiliana na wataalamu wa green agriculture kwa ajili ya ujenzi wa
green house kwa ajili ya uzalishaji bora wa strawberry.
Habari hivi kwa hapa dar ninaweza kupata wap strawbery?
ReplyDelete