KITI CHA DHAHABU CHAIBIWA
America: Wezi waiba kiti cha
dhahabu
Genge moja lilivunja na kuingia katika kasri la Oxfordshire na
kuiba kiti hicho , kulingana na maafisa wa polisi wa Thames Valley.
Kiti hicho kwa jina America , ambacho wageni wameombwa kukitumia
hakijapatikana lakini mzee mmoja mwenye umri wa miaka 66 amekamatwa.
Wizi huo ulisababisha uharibifu mkubwa kwa kuwa choo
hicho kilikuwa kimejengwa kushikana na msingi wa nyumba hiyo, polisi walisema.
Kilikuwa miongoni mwa vitu vya maonyesho ya msanii mmoja wa
Itali Maurizio Cattelan yaliofunguliwa siku ya Alhamisi.
Jumba hilo ni la karne ya kumi na nane na eneo alilozaliwa Sir
Winston Churchill. Kwa sasa limefumngwa huku uchunguzi ukiendelea.
Akizungumza mwezi uliopita nduguye wa kambo wa Churchil , Edward
Spencer alisema kwamba hakuwa na shaka kuhusu usalama wa choo hicho. ''Sio kitu
cha rahisi kufikiria''
Wageni katika jumba hilo la
maonyesho walikuwa huru kutumia vifaa vya kasri hilo kwa malengo yake huku
wakipewa muda wa dakika tatu ili kuzuia milolongo mirefu
Inspekta wa polisi Jess Milne alisema: Sanaa ilioibiwa ni kiti
chenye thamani ya juu kilichotengezwa na dhahabu ambacho kilikuwa katika
maonyesho hayo.
Tunaamini kwamba waliotekeleza kitendo hicho walitumia magari
mawili wakati wa kisa hicho.
Kiti hicho hakijapatikana lakini tunafanya uchunguzi
kukitafuta ili kuwakamata waliohusika.
Maafisa wa polisi wa Blenheim wanasema kwamba jumba hilo
litaendelea kufungwa lakini litafunguliwa siku ya Jumapili.
Rais Donald Trump aliombwa kuchukua kiti hicho mwaka 2017. Mshukiwa
kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa maafisa wa Polisi.
Comments
Post a Comment