SOKO LA MIHOGO NA KANUNI ZAKE
KILIMO BORA CHA MIHOGO : Mihogo ni miongoni mwa mazao ya mizizi ambayo ni muhimu sana kwa chakula, hasa maeneo yenye mvua kidogo na sehemu zenye ukame. Mihogo hutumika kama zao la kinga ya njaa ambapo mizizi yake hutumika kama chakula na majani yake pia hutumika kama mboga. Kutokana na baadhi ya maeneo ya nchi yetu kuwa na ukame, wataalamu wa kilimo wanasisitiza na kushauri mazao ya kinga ya njaa yalimwe. Na Mihogo ni miongoni mwa mazao hayo. Kwa hiyo basi, uangalizi wa shamba toka kuandaa shamba mpaka mavuno unatakiwa kuzingatiwa. HALI YA HEWA ,UDONGO UFAAO NA UTAYARISHAJI WA SHAMBA Ni zao linalostahimili ukame, hustawi vizuri katika maeneo yenye joto la wastani kama ya ukanda wa pwani na yale ya mwinuko usiozidi mita 1500. Ili shamba la Mihogo listawi vizuri ni vyema lilimwe kwenye ardhi yenye rutuba ya wastani, udongo tifutifu au kichanga na mvua ya wastani. Unyevunyevu ukizidi na mbolea kuwa nyingi husababisha mhogo kukua sana sehemu ya juu na kutoa majani ...
Comments
Post a Comment