MFUMUKO WA BEI YA MAFUTA
Bei ya mafuta yapanda baada ya
mashambulio dhidi ya vituo vya mafuta Saudia
Bei zilishuka kidogo baada ya rais wa Marekani Donald Trump
kuagiza kufunguliwa kwa akiba nchini Marekani.Huenda
ikachukua wiki kadhaa kabla ya vituo hivyo Saudia kurudi katika hali ya kawaida
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema
Tehran imehusika na mashambulio hayo. Iran imeishutumy Marekani kwa 'uongo'.
Baadaye Trump amesema katika ujumbe wa Twitter kuwa Marekani
inafahamu mhusika wa uhalifu huo ni nani na ipo tayari ila inasubiri kusikia
kauli ya WaSaudi kuhusu namna ambavyo inataka kulifuatilia hili.
Katika ujumbe mwingine kwenye twitter, amesema "
kuna mafuta mengi!"
Athari yake kwa usambazaji
mafuta ni ipi?
Wasaudi hawajaeleza kwa kina kuhusu mashambulio hayo, kando na
kusema kwamba hakuna aliyeathirika, lakini imetoa ishara kidogo kuhusu
utengenezaji mafuta.
Waziri wa nishati mwanamfalme Abdulaziz bin Salman amesema
kupungua kwa utengenezaji mafuta kutafidiwa kwa kutumia akiba kubwa iliopo.
Ufalme huo ndio wauzaji wakuu wa mafuta duniani, ambapo
unasafirisha zaidi ya mitungo milioni 7 kwa siku ya mafuta.
"Maafisa wa Saudia wamedai kudhibiti moto huo, lakini sio
kuwa umezimwa kikamilifu," amesema Abhishek Kumar, mkuu wa takwimu katika
shirika la Interfax Energy mjini London. "Uharibifu kwa vituo vya Abqaiq
na Khurais unaonekana kuwa mkubwa, na huenda ikachukua wiki kadhaa kabla ya
usambazaji mafuta ukarudi katika hali ya kawaida."
Saudi Arabia inatarajiwa kutumia akiba ili usafirishaji mafuta
uendelee kama kawaida wiki hii.
Hatahivyo, Michael Tran, mkurugenzi msimamizi wa mipango ya
nishati katika soko la RBC Capital Markets mjini New York, amesema: "hata
iwapo tatizo hilo litatatukiwa kwa haraka, tishio la kutenga 6% ya mafuta
yanayotengenezwa duniani sio fikra tu. Kutahitajika, faida ya ziada
inayohitajika kwa mwekezaji kujilipa."
Marekani inatuhumu nini?
Bwana Pompeo amesema Tehran imehusika na mashambulio hayo ya
uharibifu lakini hakutoa ushahidi maalum kuunga mkono tuhuma zake.
Amepinga tuhuma za waasi wa Houthi nchini Yemen wanaoungwa mkono
na Iran kwamba wao ndio waliotekeleza mashambulio hayo.
Iran imeishutumua Marekani kwa 'uongo' na waziri wake wa mambo
ya nje Javad Zarif amesema kuwa "kuituhumu Iran hakutomaliza janga"
nchini Yemen.
Yemen imekumbwana vita tangu 2015 wakati rais Abdrabbuh Mansour
Hadi alipolazimishwa na waasi hao wa Houthi kutoroka mji mkuu Sanaa. Saudi
Arabia inamuungamkono rais Hadi, na imongoza muungano wa mataifa ya kieneo
dhidi ya waasi hao.
Wakati huo huo Marekani imeituhumu Iran kwa mashambulio mengine
katika vituo vya mafuta katika enoe hilo mwaka huu, huku kukishuhudiwa wasiwasi
kufutaia uamuzi wa Trump kuidhinisha upya vikwazo baada ya kujitoa katika
makubaliano muhimu ya kimataifa yaliodhibiti shughuli za nyuklia za Tehran
Comments
Post a Comment