MWILI WA MUGABE HAUZIKWI LEO TENA
Mazishi ya Mugabe: Mwili wa
Mugabe hauzikwi leo tena
Viongozi wa Afrika wamemsifu aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert
Mugabe kama mpiganiaji wa Uhuru katika mazishi yake katika uwanja wa kitaifa
mjini Harare.
Rais wa sasa Emmerson Mnagagwa alimtaja Mugabe kama kiongozi aliyekuwa
na maono na kusema kwamba 'taifa letu linalia'.
Hatahivyo uwanja ulio na uwezo wa kubeba watu 60,000 ulikuwa na
idadi ndogo ya watu.
Uchumi wa taifa hilo upo katika hali mbaya na raia
wengi wa Zimbabwe waliamua kususia sherehe hiyo kutokana na ukandamizaji
uliotekelezwa na uongozi wa Mugabe.
Kupanda kwa hali ya mfumuko na ukosefu wa ajira ni baadhi ya
masuala ambayo yamewafanya raia wa taifa hilo kumlaumu Mugabe.
''Tunafurahia kwamba amefariki, kwa nini nihudhurie
mazishi yake? sina mafuta'', alisema mkazi mmoja wa Harare akizungumza na AFP.
''hatutaki kusikia chochote kumuhusu tena. yeye ndio sababu ya
matatizo yetu''.
Mazishi hayo yanafuatia mgogoro kati ya familia ya
Mugabe na serikali kuhusu mahala atakapozikwa.
Sasa imekubalika kwamba atazikwa katika makaburi ya mashujaa
mjini Harare, familia yake imesema.
Msemaji wa familia na mpwa wake leo Mugabe anasema kwamba hiyo
itafanyika baada ya kipindi cha mwezi mmoja wakati ambapo kaburi hilo
litajengwa katika makaburi hayo ya mashujaa .
Awali mipango ya mazishi hayo kufanyika siku ya
Jumapili ilionekana kufutiliwa mbali.
Mugabe ambaye alikuwa na umri wa miaka 95 alipofariki wiki
iliopita alikuwa akitibiwa nchini Singapore.
Viongozi wa Afrika , wa zamani na waliopo sasa
waliingia katika uwanja huo kwa shangwe kubwa pamoja na viongozi waliopigania
uhuru wa bara hili.
Rais Mnangagwa - mtu ambaye alimpindua Mugabe miaka miwili
iliopita aliketi viti viwili karibu na mkewe Mugabe Grace.
Sifa za Mugabe kama mpiganiaji uhuru zilitolewa na
kila kiongozi ambaye alisimamna kuhutubia akiwemo rais wa Kenya Uhuru kenyatta
- huku wakitofautiana na maneno yaliotolewa na mwakilishi wa familia hiyo
Walter Chidhakwa aliyesema kwamba ''Mugabe alikuwa na huzuni , huzuni mkubwa',
Ilikuwa safari ngumu na ya kuchukiza''.
Matamashi yake yalionyesha wazi wasiwasi uliopo kati ya serikali
iliopo na familia ya Mugabe.
Zaidi ya viongozi kumi wakiwemo wale wa zamani wa mataifa
ya Afrika walihudhuria mazishi hayo , wakimsifu Mugabe kama kiongozi wa Afrika
aliyeamua kutumikia maisha yake yote kwa raia wa Zimbabwe.
Rais Kenyatta alisisitiza kwamba matatizo ya Kiafrika yanahitaji
suluhu ya kiafrika.
Baadae raia wallimzomea rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
ikionekana kuwa jibu la ghasia dhidi ya wageni nchini kwake katika kipindi cha
mwezi mmoja uliopita.
Alitambua kelele hizo kwa kusema: " Katika wiki
mbili zilizopita , sisi Waafrika Kusini tumekuwa tukikabiliwa na wakati mgumu.
Tumekuwa na vitengo vya ghasia katika baadhi ya maeneo ya Afrika
Kusini...hili limesababisha kama ninavyowasikia mukisema ... vifo na majeraha
miongoni mwa idadi ya watu. lakini alisisitiza sisi Waafrika wa Kusini
hatupendi ghasia dhidi ya wageni"
Comments
Post a Comment