SOKO LA KILIMO CHA MAHINDI
Mahindi
ni miongon mwa mazao makuu ya chakula hapa nchin Tanzania na ulimwa karibu kila
mkoa. Ulimwa zaidi nyanda za juu kusini katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma,
Njimbe na Katavi. Pia mikoa ya Morogoro Mwanza Dodoma Shinyanga Arusha Tanga na
mikoa mingine. Kwakua ni zao la biashara hivyo karibu kila mkoa unalima zao
hili.
Matumizi.
Zao
hili ulimwa na utumika kwa matumizi mbalimbali yakiwemo yafuatayo
★Chakula (stample food)
★Chakula kwa mifugo
★Nishati (biofuel)
☆Dawa za asiri(mbelewele zake)
☆kutengenezea mapambo.
☆mabaki utumika kama mbolea n.k.
★Chakula kwa mifugo
★Nishati (biofuel)
☆Dawa za asiri(mbelewele zake)
☆kutengenezea mapambo.
☆mabaki utumika kama mbolea n.k.
Pia
wapo wakulima waliojikita katika kulima zao hili kibiashara ambao uuza katika
soko la ndani ya mkoa nje ya mkoa na nje ya nchi. Hapa itategemea uwekezaji wa
mkulima husika.
MAZINGIRA NA HALI YA HEWA NZURI KWA
MAHINDI
Mahindi
uota vizuri katika jotoridi lenye wastani wa 20-30 nyuzi joto za centigradi.
Pia linaitaji mvua hasa wakati wa uotaji na uotaji wa mbelewele.
MBEGU ZA MAHINDI
Kuna
aina nyingi za mbegu. Zipo za Asili na pia zipo mbegu chotara (Hybrid F1 &
F2) kutoka makampuni mbalimbali, za mda mfupi na za mda mrefu kulingana na
kipindi/vipindi vya mvua kwa mwaka kwa mkoa usika.
Kwakua
Tanzania ina kanda tofauti za hali ta hewa ikiwemo nyanda za juu kusini, nyanda
za juu kaskazini, nyanda za kati na maeneo mengine ya pwani na pia ndani ya
mkoa mmoja panaweza pakawa na matabaka tofauti yakijografia
(geographical/ecological zone).
Hivyo
mbegu za mahindi zinazofanya vizuri mikoa ya Pwani Morogoro Arusha Mwanza
haziwezi kufanya viruzi katika mikoa ya Njombe Iringa n.k kwakua utofautiana
katika ukanda.
Mbegu zinazofanya vizuri Njombe mjini ama wanging'ombe zinaweza zisifanye vizuri Ludewa ama Makete wilaya tofauti lakini mkoa mmoja.
Mbegu zinazofanya vizuri Njombe mjini ama wanging'ombe zinaweza zisifanye vizuri Ludewa ama Makete wilaya tofauti lakini mkoa mmoja.
Hivyo
ni vema kujua kua mbegu upandao inafaa kwa ukanda upi?? Wa mvua za mda mrefu!
Mda mfupi! Ama sehemu zenye ukame!!.
NAFASI
Hii
itategemea aina ya mbegu na pia namna ya utunzaji ambao utegemea sana kusudi la
ulimaji (chakula ama biashara).
UPANDAJI WA MAHINDI
Mche
hadi mche ni sm 30-40. Mstar hadi mstari ni sm 70-75.
Yaani sm 75X30, pia waweza tumia sm 80X25 punje moja moja za mbegu chotara ya mahindi.
Yaani sm 75X30, pia waweza tumia sm 80X25 punje moja moja za mbegu chotara ya mahindi.
Ni
vema ukapanda siku moja ambayo utaweka na mbolea. Anza na mbolea 5g kwa shimo
fukia kidogo kisha weka mbegu ( mbegu moja kama ni Hybrid).
Mbolea nzuri zaidi yenye maboresho na lishe linganifu kwa mmea (balanced nutrition) ni YaraMila Cereal, Yara Vera Amidas na YaraBela Sulfan kutoka kampuni ya Yara Tanzania ltd. Mfuko mmoja mmoja, utapandia, utakuzia mkuzio wa kwanza na utamalizia mkuzio wa pili kama zilivyo orodheshwa hapo.

PALIZI YA MAHINDI
Kuna
aina tatu za kupambana na magugu.
1.
Palizi la mkono/jembe.
Hili
lina gharama zaidi na linachukua mda mwingi na pia SIO SAHIHI kwakua halireti
majibu mazuri katika kuzuia magugu.
2.
Mbinu za Asiri.
Hapa
utumika matandazo kama majana makavu, majani ya mgomba, pumba za mpunga n.k (
Mulching). Huitaji kujipanga zaidi na piaupatikanaji wa matandizo wakati
wakilimo unaweza ukawa ni shida.
3.
Palizi la Dawa.
Hapa
ndio upatikana suluhisho sahihi kwa mkulima ingawa changamoto zipo katika ubora
wa dawa wingi wa madawa uwepo wa dawa feki na gharama.
Ni vema ukatumia dawa zinazotumika kuzuia magugu mara baada yakupanda kabla ya magugu kuota (somo la magugu litafuata sio mda).
Tumia PRIMAGRAM GOLD kutoka Syngenta Tanzania Ltd epuka palizi la mkono okoa mda pata faida pata mda wakupumzika na kujishughurisha na mambo mengine na uongeze kipato.

WADUDU NA
MAGONJWA KWENYE MAHINDI
WADUDU WA MAHINDI
Maize
aphids, African armyworms, Bollworm, Stalk borer, leaf hoppers.
Dawa
nzuri kuzuai hili ni Match 050EC na Karate 5EC/Karate 5CS(Originali kutoka
Syngenta epuka dawa feki ilikopiwa nembo/lebo)
MAGONJWA YA
MAHINDI
Magonjwa
ya ardhini (soil born disease), kutu ya majani n.k.
Magonjwa ya kuvu sio tatizo sana ktk kilimo hiki ingawa maeneo ya nyanda za juu kaskazini yameoneka.
Magonjwa ya kuvu sio tatizo sana ktk kilimo hiki ingawa maeneo ya nyanda za juu kaskazini yameoneka.
Tumia Artea na Amistar Kutoka kampuni ya Syngenta.
UVUNAJI WA
MAHINDI
Mda
ambao mahindi uchukua kukaa shamban hadi kuvunwa inategemea na ukanda na pia na
mbegu, mahindi ukaa wastan wa miezi mitano toka kupandwa shambani. Lakini ni
tamaduni za wakulima wengi kuacha mahindi shambani kwa mda mrefu zaidi ili
yakauke kwa matumizi ya biashara. Mahindi kwa ajiri ya gobo ukaa mda mfupi (sio
kila mbegu ni ya gobo/mahind yakuchoma) zaidi uvunwa kabla yakukomaa.
Idadi
ya gunia utazopata kwa ekari moja utegemea
→ utaratibu
uliofuatwa wakitaalum (Agronomic practices)
→ aina ya mbegu
→mazingira (ukanda)-mvua ama umwagiliaji.
→mapambano dhidi ya wadudu magonjwa na magugu.
→ usimamizi/mbolea/rutuba ya udongo wako.
Kila mbegu hasa chotara zinakua na kiasi tajwa cha mavuno kwa ekari.
Mf. Gunia 30, 25-30, ama 40 n.k. (gunia tafsiri yake kitaalum ni 100kg.

SOKO LA
MAHINDI
Soko
utegemea sana wastani ama ungezeko la walimaji na uzalishaji. Soko lake
utegemea sana watumiaji wa ndani.
Pia utokea soko katika mkampuni kama wanunuzi wadogo wadogo, kampuni ndogondogo za usagaji mahindi, taasis mbalimbali,Mohamed enterprise, Hifadhi ya taifa ya chakula, n.k na pia soko la nje ya nchi eg Kenya Uganda Sudani Ethiopia n.k

Comments
Post a Comment