SOKO LA MIHOGO NA KANUNI ZAKE
KILIMO
BORA CHA MIHOGO : Mihogo ni miongoni mwa mazao ya mizizi ambayo ni muhimu
sana kwa chakula, hasa maeneo yenye mvua kidogo na sehemu zenye ukame. Mihogo
hutumika kama zao la kinga ya njaa ambapo mizizi yake hutumika kama chakula na
majani yake pia hutumika kama mboga.
Kutokana
na baadhi ya maeneo ya nchi yetu kuwa na ukame, wataalamu wa kilimo
wanasisitiza na kushauri mazao ya kinga ya njaa yalimwe. Na Mihogo ni miongoni
mwa mazao hayo.
Kwa hiyo
basi, uangalizi wa shamba toka kuandaa shamba mpaka mavuno unatakiwa
kuzingatiwa.
Ni zao
linalostahimili ukame, hustawi vizuri katika maeneo yenye joto la wastani kama
ya ukanda wa pwani na yale ya mwinuko usiozidi mita 1500.
Ili shamba
la Mihogo listawi vizuri ni vyema lilimwe kwenye ardhi yenye rutuba ya wastani,
udongo tifutifu au kichanga na mvua ya wastani. Unyevunyevu ukizidi na mbolea
kuwa nyingi husababisha mhogo kukua sana sehemu ya juu na kutoa majani mengi.
Endapo
mihogo inaoteshwa sehemu yenye udongo wa mfinyanzi au mzito, ambao unatuamisha
maji, mihogo hushindwa kuweka Viazi itakiwavyo.
Pia sehemu
zenye mawe siyo nzuri kwani huzuia mizizi kusambaa vizuri ardhini. Pia udongo
au mchanga wenye asili ya chumvichumvi kwa wingi hufanya baadhi ya mbegu ambazo
ni mihogo mitamu kuwa na uchungu, mfano muhogo wa kiroba unaweza kuwa na
uchungu kama utachelewa sana kuvunwa kutoka katika eneo la aina hii.
AINA
Kuna aina
mbalimbali za mihogo. Baadhi ya Sifa zinazoangaliwa wakati wa kutayarisha Mbegu
za Mihogo ni;-
1.
Muda wa kukomaa
2. Mhogo
mtamu au mchungu
3. Uwingi
waavuno
·
Kibaha,
·
Aipin Valeca,
·
Msitu Zanzibar,
·
Kigoma
·
Kigoma red.
·
kiroba,
·
Binti Athumani,
·
Mzungu.
AINA YA
MIHOGO MICHUNGU NI ;-
·
Liongo,
·
Ali mtumba,
·
Mapangano,
·
Luanda,
·
mzimbatala
·
Lumbaga.
KUPANDA
Mihogo
kama mazao mengine, Mkulima hana budi kuzingatia matumizi ya mboga bora ili
aweze kupata mavuno mengi na bora.
Kwa
kawaida Mihogo hupandikizwa kwa kutumia vikonyo au pingili zinazotokana na
mihogo yenye Sifa zinazotakiwa.
Pingili
ziwe zenye urefu wa wastani wa sentimita 25-30 na wastani wa macho 5-6, na
unene wa sentimita 2-4. Mara nyingi sehemu ya shina ndiyo inayofaa kukata
pingili.
Katika
kilimo cha sesa, nafasi zinazopendekezwa ni meta 1 kwa meta 1. Katika kilimo
cha Matuta nafasi zinazopendekezwa ni meta 1.5 kwa meta 0.75.
Mkulima
asipande pingili changa au zilizokomaa na kuzeeka, na wakati wa kupanda
ahakikishe macho 2-3 yako ndani ya ardhi. Aisha hakikisha kuwa pingili urefu wa
sentimeta 10-15 unakuwa ndani ya ardhi.
Mkulima
apande pingili kwa kulaza, nyuzi 45 (45°) yaani kimshazari kidogo na macho
yatakayotoa machipukizi yawe yameelekea juu. Udongo ugandamizwe kudogo kwa mguu
ili pingili ishike vizuri.
PALIZI
Ipaliliwe
mapema inapokuwa hufunika ardhi hivyo majani huzuiwa kuota na kukua vizuri.
SAMADI NA
MBOLEA ZA VIWANDANI
Mihogo
hulimwa bila kutumia mbolea na inastawi vizuri hata katika udongo usio na
rutuba ya kutosha, Matumizi ya mbolea za nitrogeni hayashauriwi katika kilimo
cha muhogo labda kama unataka majani na si muhogo.
MAGONJWA
Zao la
mhogo halina magonjwa mengi lakini ugonjwa wa “Cassava Mosaic” na Batobato
ndiyo yanayoathiri sana uzalishaji wa zao hili. Ugonjwa huu husababishwa na
virusi na huenezwa na nzi wadogo weupe. Mmea ulioathirika ukitumika kwa vipando
mche mpya nao utakuwa na ugonjwa huu. Majani ya mmea ulioshambuliwa yatakuwa na
rangi ya njano na yasiyo na umbo la kawaida.
Kuzuia
ugonjwa huu-panda aina ya muhogo inayostahimili ugonjwa huu, Panda vipandikizi
ambavyo havijatoka katika mmea ulioathirika na ugonjwa huu, pia unaweza
kuchovya mbegu ulizokata katika maji ya moto kwa muda mfupi na kwa tahadhari
kubwa. Pia tumia dawa za wadudu kuua nzi weupe.
WADUDU
Mdudu
hatari wa mihogo ni ” Cassava green mite” ( Buibui wa mhogo) ambaye hupunguza
mavuno kwa asilimia 40 – 80.
Wadudu
wengine ambao wameonyesha madhara makubwa ni cassava mealy bugs ( vidung’ata)
ambao wameleta madhara makubwa katika maeneo yalimayo mihogo.
MIHOGO
ILIYOSHAMBULIWA NA WADUDU HAWA ITAONYESHA DALILI ZIFUATAZO ;-
1.
Shina la mmea huonekana limezungukwa
na utando mweupe (white mealy wax)
2. Kunyauka
kwa majani ya mmea.
3. Mmea hudumaa
4. Shina la
mmea huonekana limepinda
5. Majani ya
mmea hupukutika
6. Mmea hufa.
Wadudu
hupenda kushambulia majani machanga hasa Yale ya ndani ambako mmea huendelea
kukua.
TIBA ZA
KUTUMIA WADUDU
Kutokana
na utafiti, wadudu Hawa wanaweza kuangamizwa kwa njia ya Asili (Biological
control). Wataalamu waliagiza manyigu kutoka nje ya nchi pale tu ugonjwa huu
iliposhamiri lakini njia hii ilionekana ni gharama kwa Mkulima wa kawaida.
Kinachoshauriwa
ni kupanda Mbegu ambazo hazijashambuliwa na magonjwa.
Zuia
wadudu hawa kwa dawa za wadudu kama vile DIMETHOATE, n.k
MOJAWAPO YA DAWA NI CLICK HAPA >> >>>>https://www.digistore24.com/redir/348520/amoc49/
MUDA WA
KUKOMAA.
Muda wa
kukomaa unatofautiana kutokana na aina ya mhogo. Ila mihogo mingi huanzia miezi
sita hadi tisa na kuendelea
UVUNAJI
Ikiwa
mihogo yako imekomaa ing’oe yote au chagua unayoitaka kuvuna.Epuka kuweka
kidonda katika muhogo unaovuna ili kuepusha kuoza kwa urahisi.
Comments
Post a Comment