VIONGOZI WA AFRICA KUAGA MWILI WA MUGABE






Rais wa sasa Emmerson Mnagagwa alimtaja Mugabe kama kiongozi aliyekuwa na maono na kusema kwamba 'taifa letu linalia'.
Hatahivyo uwanja ulio na uwezo wa kubeba watu 60,000 ulikuwa na robo ya idadi hiyo.
Uchumi wa taifa hilo upo katika hali mbaya na raia wengi wa Zimbabwe waliamua kususia sherehe hiyo kutokana na ukandamizaji uliotekelezwa na uongozi wa Mugabe.
Kupanda kwa hali ya mfumuko na ukosefu wa ajira ni baadhi ya maswala ambayo yamewafanya raia wa taifa hilo kumlaumu Mugabe.
''Tunafurahia kwamba amefariki, kwa nini nihudhurie mazishi yake? sina mafuta'', alisema mkaazi mmoja wa Harare akizungumza na AFP. ''hatutaki kusikia chochote kumuhusu tena. yeye ndio sababu ya matatizo yetu''.
Kulikuwa na jua , na raia wachache waliokuwepo kumpatia mkono wa burihani Robert Mugabe.
Wakati ambapo jeneza ambalo lilikiuwa likimbeba mwanzilishi wa taifa hilo lilipoingia uwanjani ilikuwa wazi kwamba ni idadi ndogo walihudhuria sherehe hiyo ya mazishi.
Viongozi wa Afrika , wa zamani na waliopo sasa waliingia katika uwanja huo kwa shangwe kubwa pamoja na viongozi waliopigania uhuru wa bara hili.
Bwana Mnangagwa - mtu ambaye alimpindua Mugabe miaka miwili iliopita aliketi viti viwili karibu na mkewe Mugabe Grace.
Sifa za Mugabe kama mpiganiaji uhuru zilitolewa na kila kiongozi ambaye alisimamna kuhutubia akiwemo rais wa Kenya Uhuru kenyatta - huku wakitofautiana na maneno yaliotolewa na mwakilishi wa familia hiyo Walter Chidhakwa aliyesema kwamba ''Mugabe alikuwa na huzuni , huzuni mkubwa', Ilikuwa safari ngumu na ya kuchukiza''.
Matamashi yake yalionyesha wazi wasiwasi uliopo kati ya serikali iliopo na familia ya Mugabe.
Description: Presentational grey line
Zaidi ya viongozi kumi wakiwemo wale wa zamani wa mataifa ya Afrika walihudhuria mazishi hayo , wakimsifu Mugabe kama kiongozi wa Afrika aliyeamua kutumikia maisha yake yote kwa raia wa Zimbabwe.
Bwana Kenyatta hakusita katika matamshi yake aliposema kwamba matatizo ya Kiafrika yanahitaji suluhu ya kiafrika.
Baadaye raia wallimzomea rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ikionekana kuwa jibu la ghasia dhidi ya wageni nchini mwake katika kipindi cha mwezi mmoja uliokwisha.
Alitambua kelele hizo kwa kusema: Katika wiki mbili zilizopita , sisi Waafrika Kusini tumekuwa tukikabiliwa na wakati mgumu .
Tumekuwa na vitengo vya ghasia katika baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini...hili limesababisha kama ninavyowasikia mukisema ... vifo na majeraha miongoni mwa idadi ya watu. lakini alisisitiza sisi Waafrika wa Kusini hatupendi ghasia dhidi ya wageni

Je Mugabe atazikwa wapi?
Mazishi hayo yanafuatia mgogoro kati ya familia ya Mugabe na serikali kuhusu mahala atakapozikwa.
Sasa imekubalika kwamba atazikwa katika makaburi ya mashujaa mjini Harare, familia yake imesema.
Msemaji wa familia na mpwa wake leo Mugabe anasema kwamba hiyo itafanyika baada ya kipindi cha mwezi mmoja wakati ambapo kaburi hilo litajengwa katika makaburi hayo ya mashujaa .
Awali mipango ya mazishi hayo kufanyika siku ya Jumapili ilionekana kufutiliwa mbali.
Mugabe ambaye alikuwa na umri wa miaka 95 alipofariki wiki iliopita alikuwa akitibiwa nchini Singapore


Mjue Mugabe kidogo
Mwaka 1980, Bw Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu


Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali
Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake
Mwaka 1987,alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake
Uchumi ulidororeka baada ya mwaka 2000…
Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara ya uchumi
Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai
Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi
Ndoa yake na Grace Mugabe ,anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza
Wengi walikasirishwa na Grace kuandaliwa kuwa mrithi wake.





Comments

Popular posts from this blog

KILIMO BORA CHA NYANYA NA SOKO LAKE

SOKO LA MIHOGO NA KANUNI ZAKE

SOKO LA TIKITI MAJI NA KILIMO CHAKE