APPLE NA IPHONE 11,PRO NA PRO MAX
Kwa Apple tarehe 10 Septemba 2019
ilikuwa ni siku ya kutambulisha simu zao mpya – iPhone 11, ila sehemu kubwa ya
utambulisho huo ulihusisha zaidi huduma zake zingine mbalimbali.
Katika tukio hilo lilifanyika katika
makao makuu ya kampuni hiyo Cupertino, Apple walitambulisha kwa undani huduma
zao za Apple TV, iPad, iPhone 11, mfumo wa magemu wa Apple Arcade, na saa mpya
ya Apple Watch Series 3.
Saa ya Apple Watch Series 3
Wametambulisha toleo jipya la saa ya Apple Watch Series 3.
Kikubwa hapa ni kwamba saa hizo zimepunguzwa bei kutoka dola 279 (zaidi ya Tsh
600,000/=) na sasa toleo hili jipya litapatikana kwa dola 200 tuu (takribani
Tsh 430,000/=)
Huduma ya
Apple TV+
Huduma ya kutazama vipindi kwa mfumo wa mtandao, mpinzani
wa huduma ya Netflix, Apple TV+ itaanza kupatikana Novemba na itagharimu dola
4.99 kwa mwezi (Takribani Tsh 11,000/=)
iPad mpya ni takribani Tsh 700,000
Pia Apple wametambulisha iPad mpya ya ukubwa wa display wa
inchi 10.2. Wameongezea uwezo mzuri wa iPad kutambua na ufanyaji kazi wa
keyboard za Bluetooth. Pia kuna utumiaji wa kalamu spesheli unaweza kutumika
hasa hasa kwa kwa matumizi ya uchoraji n.k. iPad mpya inaanza kwa bei ya dola
329 za Kimarekani.
Apple Arcade
Apple wamekuja pia na huduma na mfumo wa magemu
unaotambulika kama Arcade. Kupitia malipo ya dola 5 kwa mwezi (Takribani Tsh
11,000/=) mtumiaji ataweza kucheza magemu ya aina mbalimbali bure kwenye iPhone
au iPad. Hadi sasa Apple wamesema mfumo huo una magemu zaidi ya 100.
iPhone 11.
Kama utakuwa umegundua kwa sasa moja ya vita kubwa kiushindani
katika simu janja ni eneo la kamera. Simu ya iPhone 11 inakuja na mfumo
unaotumia kamera mbili zote zikiwa ni za megapixel 12 kila moja. Kamera hizi
kwa pamoja zinahakikisha picha zinakuwa katika ubora mzuri ata kama ni picha
ambazo zinahusisha sehemu pana sana (wide & ultra-wide).
Ata kamera ya selfi pia ni ya pixel 12 ila kwa
mara ya kwanza kwa iPhone utaweza kurekodi video za 4K kwenye kamera ya
selfi. Simu hii itaanza kupatikana kwa bei ya dola $699
(Takribani Tsh 1,600,000/=).
iPhone 11 Pro na iPhone 11 Pro Max
Ukiacha toleo la iPhone 11, kuna matoleo
mengine mawili mengine..nayo ni iPhone 11 Pro na iPhone 11 Pro Max. Simu hizi
mbili ni simu ambazo wamezipa uwezo mkubwa sana wa kiutendaji kiasi ya kwamba
Apple wanaamini zina nguvu/uwezo mkubwa kiutendaji kuliko ata laptop nyingi
zinazopatikana sokoni kwa sasa. Hii ni kutokana na utumiaji wa chip/prosesa yao
mpya kabisa ya A13, pia nje ya zile kamera mbili kama kwenye toleo la iPhone
11, hizi simu mbili zinakuja na kamera ya tatu inayozidi kuongeza ubora wa
picha zake (telephoto lens).
Display ya simu hizi ni ya kiwango cha juu ya
4K – teknolojia na kiwango walichokipa jina la Super Retina OLED. iPhone 11 Pro
ikiwa na display ya inchi 5.8 wakati iPhone 11 Pro Max ikiwa na display ya
inchi 6.5.
Comments
Post a Comment