YOUTUBE WITH FAKE VIDEOS
Matangazo ya uongo ya video za matibabu ya saratani kunufaisha mtandao wa Youtube Uchunguzi uliofanywa na BBC, umebaini kuwa kuna video za lugha mbalimbali katika chaneli za Youtube, zinazotoa taarifa ambazo sio sahihi za matibabu ya saratani. Na matangazo mengine yanayoongoza kwa taarifa za uongo ni video za bidhaa mbalimbali na vyuo vikuu. Katika lugha 10 zilizopo Youtube, BBC ilibaini zaidi ya video 80 ambazo zina maudhui ya afya ambayo sio sahihi haswa ya ugongwa wa saratani. Katika video 10 zilizochunguzwa tayari watu zaidi ya milioni wameangalia. Wengi walivutiwa na matangazo hayo. Tiba ambazo hazijathibitishwa ambazo zinadai kuwa vitu kama ukwaju au amira kuwa tiba. Juisi au kufunga ni miongoni mwa tiba zilizokuwa zinafundishwa katika video hizo. Watumiaji wengine wanahamasisha watu kunywa maziwa ya Punda huku wengine wakitaka watu wanywe maji ya moto. Huku hakuna hata tiba yeyote kati walizotaja imethibitishwa kitaaluma kuwa inatibu saratani. Inaonek...