FACEBOOK WANAJUA WATUMIAJE WAKE WANAPOFANYA NGONO
Facebook wanafahamu ‘watumiaji’ wake wanapofanya ngono
Je unaweza unaweza kufikiri ni vigumu Facebook kufahamu pale
watumiaji wake wanapofanya ngono? Imefahamika si vigumu, na yote yanafanikishwa
kupitia mifumo ya data za apps na huduma za matangazo ya Facebook.
Shirika linalotetea haki za watu dhidi ya
teknolojia za kisasa – Privacy International limetoa ripoti inayoonesha tovuti
maarufu ya mtandao wa kijamii ya Facebook kwamba huwa unataka kufahamu hadi
maisha ya kingono ya watumiaji wake ili kutumia data hizo kwenye huduma zake za
kimatangazo.
Apps za uzazi na kufuatilia mizunguko
ya hedhi ni maarufu sana hasa hasa kwa wanawake. Ripoti ya Privacy
International inaonesha kupitia teknolojia zake za kimatangazo za Facebook
zinazowekwa kwenye apps hizo baadhi ya apps maarufu zimekuwa zikituma (kushare)
taarifa za watumiaji wake na hali zao hii ikiwa ni pamoja na masuala ya ngono
kwenda huduma ya matangazo na data ya Facebook.
Apps za
masuala ya uzazi na kufuatilia mizunguko ya hedhi zimekuwa zikihitaji
data/taarifa mbalimbali kutoka kwa mtumiaji ili kuweza kutoa ushauri mzuri
zaidi kwa mtumiaji. Baadhi ya
data hizo zinahusisha tarehe za mizunguko ya hedhi, na pia kama mwanamke
anataka ujauzito basi atakuwa anapata ushauri wa siku za kufanya ngono na yeye
kukubali (kutick) au kukataa kama tendo hilo halilifanya – kwa kuweka taarifa
hiyo kwenye app hizo.
Apps maarufu zilizokutwa zikifanya hivyo ni pamoja na
· Maya kutoka kwa Plackal Tech
(ina zaidi ya downloads milioni 5 kwenye Google Play),
· MIA kutoka kwa Mobapp
Development Limited (downloads milioni 1) na
· My Period Tracker iliyotengenezwa
na Linchpin Health (downloads zaidi milioni 1 Google Play)
Uchunguzi wa Privacy International
umekuta data hizo huwa zinatumwa kwenda kwa baadhi ya makampuni ya kimatangazo
na hii ikiwa ni pamoja na Facebook. Iwapo mtumiaji amejiunga kwenye app husika
kwa kutumia Facebook (login with Facebook) basi Facebook wanakuwa katika nafasi
nzuri zaidi ya kumtumia mtumiaji huyo matangazo pale atakapokuwa anatumia
huduma za Facebook au za washirika wa Facebook kupitia kurushiwa matangazo
yanayohusiana na maisha yake ya kingono kwa wakati huo.
Suala hili ni uvunjifu wa sheria
mbalimbali za kimataifa katika mabara ya Ulaya na ata Marekani. Inasemekana
muda si mrefu Facebook wanaweza jikuta katika mashtaka kutoka vyombo vya
Marekani, Uingereza na Bara la Ulaya (EU).
Suala la ‘Big Data’ – mjumuhisho wa
data/taarifa mbalimbali za watumiaji wa intaneti limekuwa changamoto sana kwa
sasa. Suala kubwa likiwa ni jinsi gani ya kuhakikisha data za watumiaji wa
huduma/mitandao/apps mbalimbali zinakuwa salama na haziendi kutumika nje ya
matakwa yao.
Comments
Post a Comment