GOOGLE YAPIGWA FAINI NA UFARANSA YA $1 BILLION
Wakati
Marekani na Ufaransa wakifanya mazungumzo juu ya suala la kodi kwa makampuni ya
biashara za kimtandaoni hasa hasa ya kimarekani tayari taarifa imetoka
inayosema Google wamepigwa moja ya faini kubwa zaidi kuwahi kutolewa huko
nchini Ufaransa.
Ni miezi sasa tokea serikali ya
Marekani ipandishe kiwango cha kodi dhidi ya vinywaji vya divai (wine) vya
nchini Ufaransa vinavyoingizwa Marekani, uamuzi huo ulikuja baada ya serikali
ya Ufaransa kudai ya kwamba inataka kudai kodi nyingi kutoka kwa makampuni ya
biashara za kimtandao kama Google, Facebook, Amazon na mengineyo.
Suala hilo halikupendwa Marekani kwa kuwa
makampuni haya mengi ni ya nchini humo na huwa wanatoa ripoti zao za kifedha na
kulipa kodi nchini Marekani na hivyo uamuzi wa Ufaransa unaweza kuwa kandamizi
na kupunguza kodi kwa Marekani.
Wakati tayari serikali hizo mbili
zimesema zitafanya mazungumzo kuhusu jambo hilo wachunguzi wa masuala ya kodi
nchini Ufaransa wamefanikiwa kufikia makubaliano na Google yatakayohusisha
kampuni hiyo kulipa zaidi ya dola bilioni 1 za Kimarekani (Zaidi ya Trilioni 2
za Kitanzania).
Google wamekuwa wakiendesha biashara za bara la Ulaya kutoka
makao yao makuu ya barani humo yaliyopo Dublin nchini Ireland. Suala hili
limewafanya wasiwe wanalipa kodi katika mengine, na sasa hali itabadilika sana
kutokana na ushindi huu wa Ufaransa katika mazungumzo yake.
Biashara za mtandaoni zimekuwa zikikua
kwa kasi sana na kitu kikubwa ni kwamba hazitambui mipaka ya nchi – ni
utandawazi kwelikweli. Jambo hili linasumbua vyombo vingi vya kodi kwani malipo
na biashara za kimtandao kati ya makampuni ya taifa moja hadi jingine yamekuwa
yakikua kwa kasi.
Comments
Post a Comment