UBER KUJA KIUSALAMA ZAIDI
Kampuni
ya Uber inatarajia kuzindua sasisho lake jipya ambalo litamwezesha mteja
kusafiri kwa usalama zaidi nyakati za usiku bila wasi.
Toleo Hili litakuwa linafanyakazi kwa
njia hii hapa, Kuna muda unaweza ukawa umeagiza usafiri ukufate Ila matokeo yake unajikuta umeingia katika gari ambalo silo, Sasa ili kuepusha visanga
hivyo, Uber inaleta kitu kipya ambacho kinaitwa Pin, yaani kabla ya kuingia
kwenye gari uliloagiza likufate, unamtumia dereva pincodes, dereva zikimfikia Basi wewe utapokea Ujumbe kwamba Hilo ndilo gari
uliloagiza Ila Kama Ujumbe hautofika kwako Hilo si gari lenyewe.
Toleo hili linatarajiwa kuanza kufanyakazi majira ya
usiku tu
Comments
Post a Comment