YOUTUBE WITH FAKE VIDEOS
Matangazo ya uongo ya video za matibabu ya saratani kunufaisha mtandao wa Youtube
Na matangazo mengine yanayoongoza kwa taarifa za uongo ni video
za bidhaa mbalimbali na vyuo vikuu.
Katika lugha 10 zilizopo Youtube, BBC ilibaini zaidi ya video 80
ambazo zina maudhui ya afya ambayo sio sahihi haswa ya ugongwa wa saratani.
Katika video 10 zilizochunguzwa tayari watu zaidi ya milioni
wameangalia.
Wengi walivutiwa na matangazo hayo.
Tiba ambazo hazijathibitishwa ambazo zinadai kuwa vitu kama
ukwaju au amira kuwa tiba.
Juisi au kufunga ni miongoni mwa tiba zilizokuwa zinafundishwa
katika video hizo.
Watumiaji wengine wanahamasisha watu kunywa maziwa ya Punda huku
wengine wakitaka watu wanywe maji ya moto.
Huku hakuna hata tiba yeyote kati walizotaja imethibitishwa
kitaaluma kuwa inatibu saratani.
Inaonekana kuwa kuna video nyingi zinazotangaza tiba ya uongo ya
saratani pamoja na matangazo ya bidhaa kama Samsung na Heinz.
Matangazo yaliyopo Youtube huwa yanainufaisha kampuni ya Google
pamoja na waliotengeneza video za uongo.
Mwezi Januari , Youtube ilitangaza kuwa itaziondoa
video ambazo zina maudhui ambayo si rafiki kwa mtazamaji kwa moja ama nyingine
haswa video zinazodai kutoa tiba za miujiza kwa magonjwa hatari.
Kampuni hiyo ilijaribu kutatua tatizo kwa video za kiingereza tu
na haikutilia maanani lugha nyingine.
BBC ilifanya uchunguzi katika lugha ya Kiingereza, Kireno,
Kiarabu, kirusi, kihindi, Kifaransa, Kijerumani na Kiitaliano.
Kwa mfano katika lugha ya Urusi, watu wanahamasishwa
kunywa maji ya amira kama tiba ya kansa.
Video hiyo ilikuwa inawashauri watu kufunga kula na kunywa juisi
ya karoti .
Pamoja na kwamba Youtube imekataza maudhui ambayo yanaweza
kuleta madhara kwa binadamu kwa kuhamasisha maudhui ya uongo lakini bado
changamoto ni kubwa.
Kwa sababu inaonekana kuwa kuna wengi wanaoamini tiba hizo za
uongo na hata kutozingatia tiba sahihi.
Fedha nyingi zinapatikana katika
video zenye maudhui ya uongo
Watafiti kutoka BBC Monitoring na BBC news Brasil walikuwa
walipata athari mara baada ya video za uongo za tiba kuanza kusambaa.
Pamoja na matangazo ya kliniki, Samsung na Heinz , BBC iliona
pia matangazo ya programu za kushihisha maneno, kukata tiketi katika mitandao,
filamu za Hollywood pamoja na vyuo vikuu.
Video zote zilikuwa na taarifa zisizo sahihi.
Kampuni na Vyuo, vimejiweka mbali katika maudhui hayo ya uongo
na kudai kuwa hawana uhusiano wowote.
Wataalamu wa afya wanasema kuwa ili kupata seheme ya
suluhisho ni vyema watengenezaji wa maudhui ya afya wafanye kazi na wataalamu
wa tiba.
"Kuna umuhimu wa elimu kutolewa ili wataalamu wa afya
kufanya kazi na watayarishaji vipindi, ingawa sina uhakika kama kuna uwekezaji
wa kutosha", Mtaalamu wa afya alisema.
Comments
Post a Comment