Posts

ISRAEL:MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI HALI TETE

Image
Benjamin Netanyahu akabiliwa na hali ngumu Ripoti za matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Israel zinaonyesha waziri mkuu  Benjamin Netanyahu ameendelea kukabana koo na mpinzani wake mkubwa Benny Grantz. Vyombo mbalimbali vya habari vya Israel vimeripoti kwamba chama cha  Netanyahu  cha mrengo wa kulia cha Likud na kile cha Bluu na Nyeupe cha mpinzani wake Grantz kila kimoja kimepata viti 32 kati ya viti 120 vya bunge baada ya takriban asilimia 90 ya kura kuhesabiwa. Ripoti hizo zilinukuu duru kutoka tume ya uchaguzi kwani kiwango hicho cha matokeo kilikuwa hakijachapishwa rasmi na hakikutarajiwa kabla ya leo alasiri. Matokeo ya awali katika uchaguzi wa Israel kwa kawaida huwa si ya uhakika na huku matokeo rasmi yakitarajiwa kutolewa Jumatano, huenda bado Netanyahu akapata ushindi, ingawa vituo vyote vitatu vimeonyesha matokeo sawa. Kwa matokeo hayo, pande zote zitatakiwa kuunda serikali itakayojumuisha vyama vingine bungeni hali inayoibua uwezekano wa maz

BENJAMIN NETANYAHU AKANUSHA MADAI YA UJASUSI DHIDI YA MAREKANI

Image
Netanyahu akanusha taarifa inayodai Israel kuhusika na ujasusi dhidi ya Marekani   Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekanusha taarifa zinazodai kuwa nchi yake inaipeleleza Marekani . Ripoti hiyo imeeleza kuwa maafisa watatu wazamani wa Marekani ambao wanasema kuwa Israel ilikuwa inahusika kuweka kifaa karibu na ikulu ya Marekani. Lakini maelezo kutoka katika ofisi ya Netanyahu imekanusha kutohusika kwa namna yoyote. "Israel ina majukumu mengi ya kuyafanyia kazi nchini mwake hivyo haiwezi kujihusisha na shughuli za ujasusi nchini Marekan Rais Donald Trump, aliulizwa na waandishi wa habari siku ya alhamisi kuhusu ripoti hiyo ya ujasusi naye alisema kuwa aamini kama Israel ilikuwa inaipeleleza Marekani . "Inaniwia vigumu kuamini kuwa Israel wana tuchunguza kwa sababu tuna uhusiano mzuri," Rais Trump alisema. alisema pia kuwa mwishoni mwa majadiliano ya mkataba wa nyuklia na viongozi wa Marekani wamekuwa wakipingana katika kuhamisha ubalozi wa

RWANDA AND UGANDA KUFIKIA MAKUBALIANO KUBORESHA USALAMA

Image
Wajumbe wa serikali za Rwanda na Uganda ambao wamekutana mjini Kigali Jumatatu, wamekubaliana mambo kadha ikiwemo kujiepusha na harakati za kuyumbisha usalama katika nchi mojawapo. Katika taarifa ya pamoja iliyokamilisha kikao hicho, Rwanda imetoa orodha ya raia wake wanaozuiliwa nchini Uganda, na serikali ya Uganda imekubali kuchunguza kwa kina taarifa hiyo, na kuhakikisha wale ambao watakutwa hawana hatia kuachiliwa huru. Pande hizo zimekubaliana pia kusahihisha mkataba wa kuwarudisha makwao watuhumiwa wa uhalifu. Wajumbe kwenye mkutano huo wa mjini Kigali wamekubaliana na kuachana na tabia ya kutumia vyombo vya habari au mitandao ya kijamii, kwa kufanya propaganda ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa nchi zao. Aidha pande zote zimesema suala la uhuru wa usafiri wa watu na vitu kwenye mpaka wa nchi zao, litajadiliwa katika kikao kingine ambacho kitafanyika mjini Kampala, baada ya kipindi cha siku 30. Ujumbe wa Uganda kwenye mkutano huo wa Kigali ulikuwa unaongozwa

IRAN KUSHUTUMIWA NA MAREKANI KUSHAMBULIA HIFADHI YA MAFUTA SAUDIA

Image
Marekani yasema Iran ilikuwa nyuma ya mashambulio ya hifadhi ya mafuta ya Saudia Marekani imetoa picha za setilaiti na kunukuu taarifa za ujasusi kuthibitisha madai yake kwamba Iran ilikuwa nyuma ya mashambulio dhidi ya vituo vya mafuta vya Saudia Iran inakana kuhusika na mashambulio hayo ya ndege , ambayo yalidaiwa kutekelezwa na waasi wa kiuhudhi wanaounga mkono Iran nchini Yemen. lakini maafisa wa Marekani ambao hawakutajwa majina wakizungumza na vyombo vya habari vya kimataifa nchini Marekani wamesema eneo na ukubwa wa mashambulio vinaonyesha kuwa Wahudhi hawakuhusika na mashambuli hayo. Tukio hilo lilisababisha kupungua kwa mauzo ya mafuta duniani kwa 5% na limesababisha kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo. Marekani inasema nini ? Waziri wa ulinzi wa Marekani Mike Pompeo aliilaumu Iran wikendi bila kutoa ushahidi wowote , jambo lililoichochea serikali ya Tehran kuushutumu utawala wa Washington kwa uongo. Katika ujumbe wake alioutoa kwneye mtandao wa kijamii wa

MANCITY LEGENDS vs PREMIER LEAGE ALLSTARS

Image
Unaambiwa Samaki anakufa na utamu wake

MAGUFULI;JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI LILITELEKEZWA

Image
Rais John Magufuli aahidi kutekeleza miradi ya maji Singida Mashariki Raisi wa Tanzania John Magufuli amesema jimbo la Singida Mashariki lilikuwa limetelekezwa bila ya uwakilishi wa mbunge. Tundu Lissu, kutoka chama cha upinzani cha Chadema alichaguliwa kuliongoza jimbo hilo kwa mara ya pili 2015, lakini toka Septemba 7, 2017 amekuwa nje ya Tanzania kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Katika kipindi chote hicho, jimbo hilo limekuwa wazi bila ya mwakilishi bungeni. "Saa nyengine majimbo yanakosa uwakilishi...Kama ulivyoagiza mheshimiwa Spika (Job Ndugai) kwamba tushughulikie tatizo la maji katika jimbo lile…kama tulivyoshughulikia jimbo la Dar es Salaam…ninakuahidi kwamba serikali yangu itashughulikia, ili yale yaliyokuwa yamechelewa yaanze kufika haraka haraka," amesema Magufuli. Mwezi Juni mwaka huu alifutwa ubunge rasmi na Spika Job Ndugai amabaye alitaja sababu kuu mbili za kufanya uamuzi huo. Sababu ya kwanza ilotajwa

MFUMUKO WA BEI YA MAFUTA

Image
Bei ya mafuta yapanda baada ya mashambulio dhidi ya vituo vya mafuta Saudia Gharama ya mafuta imepanda kwa kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa katika miezi minne baada ya mashambulio mawili dhidi ya vituo vya mafuta Saudi Arabia Jumamosi yaliosababisha kumwagika kwa 5% ya mafuta duniani. Kiwango cha mafuta ghafi yalipanda kwa 19% kwa thamani ya $71.95 kila mtungi huku viwango vingine, West Texas Intermediate, vikipanda 15% kwa thamani ya $63.34. Bei zilishuka kidogo baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuagiza kufunguliwa kwa akiba nchini Marekani. Huenda ikachukua wiki kadhaa kabla ya vituo hivyo Saudia kurudi katika hali ya kawaida Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema Tehran imehusika na mashambulio hayo. Iran imeishutumy Marekani kwa 'uongo'. Baadaye Trump amesema katika ujumbe wa Twitter kuwa Marekani inafahamu mhusika wa uhalifu huo ni nani na ipo tayari ila inasubiri kusikia kauli ya WaSaudi kuhusu namna ambavyo inataka kulifuatilia hi